Nahodha mmoja wa boti za kitalii katika jimbo la Florida aliyenyofolewa mkono na mamba anakabiliwa na mashitaka kwa kosa la kujaribu kumlisha mamba huyo.
Rekodi katika mahakama ya Collier zinaonyesha kuwa nahodha huyo Wallace Weatherholt ameshitakiwa kwa kumpa chakula mamba huyo kinyume cha sheria.
Kesi ya nahonda huyo mwenye umri wa miaka 63 inatarajiwa kutajwa tena Agosti 22 mwaka huu.