Ofisa kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Thabit Matotola (wa pili kushoto) akiwaelimisha wananchi leo majukumu ya Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Ofisa kutoka Dhamana ya uwekezaji Tanzania(UTT) Mvumo Balati (kushoto) akiwaelimisha Polisi faida kuwekeza katika mfuko huo leo mjini Dodoma wakati walitembelea maonyesho ya nanenane mjini Dodoma kwenye banda la Wizara ya Fedha.
Ofisa Operesheni wa Mfuko wa Pesheni ya Watumishi wa Umma (PSPF) Kahenga Maulid (kushoto)akijibu maswali mbalimbali ya mwananchi huyo aliyetaka kujua majukumu ya mfuko katika kumsaidia mtumishi umma wakati wa maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma leo.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Idara ya Kuondoa Umaskini William Ghumbi (KUSHOTO) akiwaelimisha wananchi juu ya MKUKUTA II walipotembelea  banda la Wizara ya Fedha leo mjini Dodoma kwenye maonyesho ya nanenane .(Picha na HAZINA-Dodoma).