StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 4, 2012

Clinton:"Khartoum na Juba pataneni"

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

JUBA KHATOOM PATANENI, WAZIRI CLINTON WA MAREKANI AASA

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton amezitaka Sudan na Sudan Kusini kumaliza uhasama baina yao. Akizungumza mjini Juba amesema uhasama ambayo ulizifanya nchi hizo mbili zikaribie vita hazifai kwa nchi ambazo ni jirani.
Bi Clinton ndiye afisa wa kwanza wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kuzuru nchi hiyo tangu ijipatie uhuru Julai mwaka jana.
Makataa iliyowekwa na Umoja wa Mataifa ya kutaka nchi hizo mbili kumalizi tofauti zao kuhusu malipo ya upitishaji wa mafuta ilikamilika jana.
Sudan Kusini ndio nchi ya pili ambayo Bi Clinton anazuru katika ziara yake ya mataifa saba ya bara Afrika.
Waziri huyo aliwasili Juba majira ya alasiri akipitia Senegal akitokea ,Uganda.
"Ijapo Sudan na Sudan Kusini sasa ni nchi tofauti lakini maendeleo yao yanategemea uhusiano kati yao," alisema baada ya kukutana na Rais Salva Kiir was Sudan Kusini.
"Ni jambo la dharura kwa nchi hizi mbili, Kaskazini na Kusini, kuendelea kujadiliana ili muafaka kuhusu utata baina yao uweze kupatikana.
"Kila moja ya nchi hizo ni sharti zilegeze misimamo yao iliklupunguza uhasama kati yao"
Matamshi ya Bi Clinton akiwa Senegal yaliolaumu sera za serikali ya China kuhusu sera zake barani afrika matamshi yake yameshutumiwa na vyombo vya serikali ya China.
Katika taarifa yake mjini Dakar Bi Clinton alisema Marekani inazingatia zaidi mfumo wa uhusiao wenye manufaa kulko ule wa kunyonya raslmali.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat