Kamati
ndogo iliyoundwa na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu
kupigania haki ya kufunguliwa kwa gazeti la MwanaHalisi, leo imeipa
serikali siku saba kuliruhusu gazeti hilo kuendelea kuchapishwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo
Bwana Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya
jambo hilo kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani.
Kamati
hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia imeitaka serikali
kutekeleza madai mbalimbali ikiwemo kulifungulia gazeti la Mwanahalisi
maramoja.
Aidha
kamati hiyo imeitaka serikali badala ya kushughulikia Watetezi wa haki
na wanahabari wanaofichua uovu, ishughulike na wahalifu waliomteka Dkt.
Stephen Ulimboka.
Gazeti la mwana halisi limefungiwa na Serikali kwa muda usiojulikana, kutokana na taarifa iliyotolewa na gazeti hilo toleo namba 304 kuhusu mawasiliano
ya mwana usalama Ramadhani Ighondu, na namba zake za simu zote ambazo
alikuwa akifanya mawasiliano na Dr. Ulimboka na watu mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!