
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga akiondoka baada ya mahakama kutengua wake wa kiti cha ubunge.
Mahakama
ya Tabora leo imetengua ushindi wa kiti cha Ubunge wa jimbo la Igunga,
Tabora kilichokuwa kinakaliwa na Dkt. Peter Dalaly Kafumu (CCM).
Kesi
dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa
kiti hicho kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mwalimu Joseph Kashindye.
Katika kesi hiyo Bwana Kashindye amewashitaki
Dkt. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema
na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi jimboni humo, Bw. Protace Mgayane.
Aidha imeelezwa kuwa Bwana
Kashindye amewashitaki kuwa wakati wa kampeni, watuhumiwa walitoa
vitisho, ahadi ya ujenzi wa Daraja la Mbuntu na kugawa mahindi.
Akizungumza
na waandishi wa habari hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Nzega, Bwana
Silvester Kainda, amesema awali Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, ilipanga
kutoa hukumu Agosti 20, mwaka huu lakini kwa bahati mbaya siku hiyo
ilikuwa ni sikukuu hivyo ikaahirishwa hadi leo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!