Rais
Jakaya Mrisho kikwete akizindua mpango wa kugawa Ng’ombe 1500 kila
mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jashp
cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake
mwaka 2008/2009.
Rais
Jakaya Kikwete akimkabidhi Ng’ombe mmoja wa wakaazi wa Monduli
walioathririka na na ukame mwaka 2008/2009 ambapo walipoteza mifugo yao
yote. Hafla hii imefanyika leo Monduli.
Rais
Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani
Monduli mchana wa leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng’ombe
1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama
kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na
athari zake mwaka 2008/2009.
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani
Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500
kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta
jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari
zake mwaka 2008/2009.(Picha na Ikulu).
SERIKALI itakuwa inagawa
ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha
kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000
iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Ahadi hiyo imetolewa leo,
Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa
Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya
Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.
Katika uzinduzi huo
uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na
wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la
kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa
kaya 16 za mwanzo.
Uzinduzi huo ni wa pili
kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake
kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni
12.9.
Februari 19, mwaka huu, Rais
Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye
sherehe zilizofanyika mjini Loliondo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!