StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 20, 2012

AJALI NYINGINE TENA YATOKEA JANA JIONI ARUSHA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Hii ni gari aina ya Hiace ya abiria ambayo inafanya safari zake kutokea Usa mpaka Arusha mjini, ilikuwa imepata ajali eneo la Makumira katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.


Huyo aliyevaa nguo za rangi ya dark blue ndio kondakta wa Hiace iliyoppta ajali.



Hawa ni baadhi ya watu waliokuwa eneo la ajali wakiangalia ajali ilivyo tokea na kudadisi chanzo cha ajali hiyo


Hii ndio tairi ya mbele ya gari iliyopasuka na kusababisha ajali.
.
Hii ndio gari aina ya Harrier ambayo ilitokea Arusha mjini ikielekea Usa, ikapasuka tairi ya mbele na kupata ajali eneo la Makumira katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.


Hawa ni baadhi ya askari wa usalama barabarani wakiwa katika eneo la ajali.


MAJIRA ya saa kumi jioni imetokea ajali mbaya katika eneo la Makumira wilayani Arumeru mkoani arusha baada ya gari aina ya Harrier yenye nambari ya usajili T225 BGK kupata pancha na kukosa muelekeo na kuenda kugoga Hiace ya abiria yenye nambari za usajili T147 BGQ inayofanya safari zake kutoka Usa kwenda Arusha mjini.
Baada ya Harrier hiyo kugonga Hiace ni kwamba Hiace hiyo ili anguka na kusababisha abiria walio kuwepo ndani ya Hiace hiyo kuumia sana lakini mpaka tunafika kwenye eneo la ajali hakuna hata abiria mmoja aliye fariki.
Mmiliki wa Harrier ni Bwana mmoja aliyejitambulkisha kwa jina laMwanga ambaye anafanya kazi katika kampuni ya uchimbaji wa madini (Tanzanite One) lililopo Mirerani, na kwa muda huo ndio alikuwa akielekea Usa kupaki gari yake hiyo ambapo baada ya hapo alikuwa ameshawasiliana na rafiki yake anayeitwa Shujaa ili aweze kumpeleka kibaruani (Tanzanite One).
Mpaka tunaondoka kwenye eneo la ajali hatukufanikiwa kumuona dereva wa Hiace wala mmiliki wa Hiace

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat