Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la
utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven
Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu
ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema
ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa
msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa
taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua
maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo
maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara,
kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote
watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria
itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo