Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (shoto) akimkabidhi msanii Ambwene Yessayah (AY) simu aina ya Sumsung Galaxy mara baada ya kumtangaza AY kuwa Balozi wa Airtel kwa Upande wa wasanii nchini Tanzania
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtangaza Balozi wake mpya kwa mwaka 2012-2013 ikiwa ni utaratibu iliyojiwekea katika kushirikiana na wasanii nchini ili kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
AY ni msanii mahiri nchini kwenye muziki wa kizazi kipya aliyejipatia heshima na kuvuta hisia za wapenda burudani wengi pale anapokuwa jukwaani, AY alijulikana zaidi baada ya kuachia album yake ya kwanza iliyobeba wimbo mkali wa ‘Raha kamili” na kufanya apendwe zaidi kitaifa na kimataifa kuanzia mwaka 2001
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeingia makubaliano na msanii AY kuwa Balozi wetu wa mwaka huu, lengo letu ni kuendelea kuwa karibu zaidi na wasanii wetu nchini na pia kufanya nao shughuli za kijamii ili kufaidisha taifa letu kwa kuwa wasanii wetu ni mahiri zaidi na wote tunafahamu AY ni msanii mkongwe na anayejituma, hivyo tunaamini ushirikiano huu utaweza kutimiza malengo yetu
ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhudumia jamii kupitia miradi mbali mbali ya jamii inayoendeshwa na Airtel pamoja na kuiwakilisha Airtel kwa kuwa Balozi mzuri.
“Sasa AY atakuwa ni msanii wa pili kuingia mkataba kama huu ambapo mwaka uliopita alikuwa Ali Kiba. Tulimtangaza Ali kiba kuwa Balozi wa Airtel mwaka jana na ameshirikiana na Airtel kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kuitangaza Airtel kupitia matangazo ya radio, Luninga, Mabango na Mabandiko lakini pia alifanikiwa kuiwakilisha nchi yetu kwenye wimbo wa Hands Across the World alioimba na wasanii wengine wa kimataifa akiwemo R.Kelly katika kundi la One8 kwa udhamini wa Airtel na kufaulu sana kubainisha umahiri wa wasanii wa Tanzania kwenye mataifa mengine makubwa kupitia kazi yake nzuri aliyofanya ndani ya wimbo huo”aliongeza Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kati) akimtangaza msanii Ambwene Yessayah (AY) (shoto) kuwa Balozi wa Airtel Tanzania kwa Upande wa wasanii nchini Tanzania kwa mwaka 2012 -2013
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!