StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

October 31, 2012

HILI NDILO TUKIO ZIMA LA WANAFUNZI WA SEKONDARI WALIONDAMANA JANA WAKAPIGWA MABOMU NA KUOKOTA MOJA LIKIWA HALIJALIPUKA MJINI ARUSHA JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
KAMANDA wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla, akiwa amemnyang'anya bomu
hilo, mwanafunzi huyo, baada ya kuonyesha, huku akisikika akisema
halijalipuka na ni hatari kuendelea kulishika, sababu lilianguka kwa
bahati mbaya


MMOJA wa wanafunzi hao ambaye hakujulikana jina lake mara moja, akiwa
anaonyesha wenzake bomu linalodaiwa kutolipuka, mbele ya Mkuu wa Mkoa
Arusha,ambalo alidhani ni ganda limeangkuka baada ya kulipuka.


WANAFUNZI wakiwa mbele ya jengo la Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa
mulongo, wakimsubiri kumpa malalamiko yao.

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kimnyaki, Wilayani Arumeru, wameandamana wakiwa na mabango mbalimbali hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na kusababisha vurugu kubwa kutokea barabara ya Ngaramtoni, nje kidogo ya Jiji la Arusha, hali iliyolazimisha jeshi la Polisi kutumia nguvu kwa kuwatawanya kwa kuwapiga mabomu ya machozi.

Aidha katika vurugu hizo, mmoja wa wanafunzi aliokota bomu lililokuwa halijalipuka, akidhani kuwa ni ganda la bomu lililotumika, huku akimwonyesha mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, hali iliyosababisha Kamanda wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla kumnyang’anya haraka, kabla ya kuleta madhara.

Maandamano hayo yalikuwa ya kushikiza kufukuzwa kwa Mwalimu Mkuu wa shule Marium Chamle kwa sababu ya kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha nne kutoingia chumba cha mitihani.

Blog hii ilishuhudia wanafunzi hao katika hali isiyo ya kawaida kila mmoja alikuwa na chupa ya maji, ambayo walikuwa wakinawa wakati wa mabomu hayo na kusonga mbele hadi ofisi hizo. Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa mulongo,kwa niaba ya wenzake, Mesharck Lomnyaki alisema mwalimu mkuu huyo amesababisha baadhi wa wanafunzi wa kidato cha nne kuchelewa kufanya mitihani yao ya baraza la mitihani (NECTA), kwa kuzuia kuingia katika chumba cha mitihani toka saa mbili asubuhi na kuwaruhusu kuingia saa 4.30.

Aidha alisema Oktoba 16 mwaka huu, walinyimwa mwongozo wa kujibu swali la tano, lenye alama kumi, kwenye somo la Chemia , ambao hawakupata kulingana na muda na kusababisha usumbufu ndani ya chumba cha mtihani na kusababisha kukata tamaa kwenye somo la Fizikia. Pia alidai tatizo la kufanana na hilo limejitokeza kwa wanafunzi wa kidato cha pili, kwenye mtihani wa Moko, ambapo aliwafukuza wanafunzi hao kutomaliza mtihani huo, kwa sababu ya kutolipa michango na kusababisha wanafunzi 46 kutofanya kabisa mtihani huo. Alisema matokeo ya kuzuia wanafunzi hao yalisababisha kushuka kwa
kiwango cha ufaulu, hali iliyosababisha mwalimu huyo kutoa lugha za kashfa na kujenga woga kwa wanafunzi  hao wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili, utakaofanyika mwaka huu.
“Lakini tunasikitika badala ya kutusikiliza kero zetu, Polisi wanatupiga mabomu barabarani ili tusiandamane na baadhi yetu tumeokota ganda hili hapa la bomu,”alisema Mara baada ya kuonyesha ganda hilo, ndipo Kamanda wa Oparesheni Maalum, Peter Mvulla, aliposhituka na kumnyang’anya bomu mtoto aliyeshika, akidai hilo lilikuwa ni bomu halikulipuka na lilikuwa na hatari ya kulipuka endapo lingeshikwa shikwa kwenye chuma maalum cha kushitua.
Alisema bomu hilo lilianguka kwa bahati mbaya, katika vurugu za kuwatuliza kuandamana, ambapo wanafunzi hao waliwapiga mawe Polisi hao na kulazimisha kutumia nguvu ndogo tu ya kujaribu kuwatuliza, lakini hawakusikia, waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Naye mwanafunzi mwingine Ezekiel Memiri, alitaja kero zingine kuwa ni unyanyasaji wa wanafunzi, ambapo wengi hufukuzwa kwa makosa madogo
madogo, bila udhibitisho wa bodi ya shule. “Hili limesababisha wanafunzi aidi ya 20 kufukuzwa shule na baadhi kusimamishwa na baadhi ya waalimu kuwatumikisha wanafunzi majumbani mwao kwa kuwafulia nguo hadi za waume zao,”alisema.
Alisema kutokana na hilo wameomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati na kumbadilisha Mkuu wa shule hiyo kwa sababu matokeo yao yanazidi kushuka kitaaluma. Naye Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo, aliwasikilia wanafunzi hao, huku akigeuka kuwa mbogo na kuamuru Polisi kukamata wanafunzi wao wawili waliokuwa wanatoa maelezo kwa niaba ya wenzao ambao ni Mesharck Lomnyaki na Daudi aliyeptikana jina moja, kwa madai wao ndio viongozi wa maandamano hayo .
Alisema kuwa kwa sasa anashangaa kumezuka tabia ya wanafunzi shuleni Mkoani Arusha kuandamana hata kwa makosa yasio na sababu hadi ofisini kwake jambo ambalo amelikemea na kutoa onyo kwa shule zote Mkoani hapo kuacha tabia hiyo vinginevyo atazifungia. “Shule zitakazoandamana kuanzia leo nitazifungia ili mkose kabisha masomo, maana hamtaki kusoma na leo ningefanya hivi, lakini nimeonea huruma watoto wa kike walio wengi ambao tunapigania wapate elimu, ila hawa viongozi wenu wapelekwe ndani iwe fundisho la tabia hii,”alisema. Mulongo alitoa hadi kufika saa tisa jioni ya jana, wanafunzi hao wawe wamerejea shuleni kwao, kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Elimu, vinginevyo atawafungia shule yao.

“Nashangaa kupigwa mabomu, mnashangaa nini wakati mmeandamana bila kibali, mlitegemea nini mnavunja sheria na mkivunja sheria kwa kudai haki, hata haki mnayotaka hamtapata,sababu ya kuvunja sheria”alisema.

Hata hivyo ilichukua muda wanafunzi hao kutawanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa, wakishinikiza kuachiwa kwa wenzao wawili waliokamatwa na Polisi, hadi pale Polisi walipoamua kutoweka kwa gari namba PT. 1834 na kuwaacha kwenye mataa wanafunzi hao wakibaki hawana cha kufanya,zaidi ya kuondoka hadi makao Makuu ya Polisi kusubiri wenzao kuachiwa.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat