BAADHI ya wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa Musica juzikati wamepata ajali ya gari na kusababisha kuumia sehemu mbalimbali za mwili huku wakidai ajali hiyo ni ya pili ndani ya siku saba.
Ajali hiyo iliyotokea Septemba 2, mwaka huu maeneo ya Msasani jirani na Ubalozi wa Marekani, ilitokana na gari walilokuwemo wanamuziki hao kugonga ukuta wakati wakitokea kwenye shoo Kawe, Dar.
Ajali nyingine ilitokea Alhamisi ya Agosti 30, mwaka huu maeneo ya Magomeni ambapo gari lao liligonga nguzo ya umeme wakati wanamuziki hao walipokuwa wakitokea Ukumbi wa Sun Cirro, Ubungo, Dar walikokuwa wakifanya shoo. Hakuna aliyeumia katika ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!