StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 6, 2012

TENDWA ATISHIA KUKIFUTA CHAMA CHOCHOTE KINACHOCHOCHEA MACHAFUKO NCHINI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Kutokana na kuendelea kwa mfululizo wa matukio mbalimbali yanayosababishwa na vurugu za kisiasa kati ya baadhi ya vyama vya siasa dhidi ya jeshi la polisi, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania imesema imechoshwa na matukio hayo ambayo yamekua yakisababisha vifo vya mara kwa mara kwa raia wasio na hatia.

Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amesema ofisi yake kuanzia sasa imepanga kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kukifuta chama chochote cha siasa kitakachothibitika kufanya mkutano kinyume cha sheria na kusababisha vurugu pasipo kujali kama vurugu hizo zimedhuru au hazijadhuru raia yeyote.

Vilevile Tendwa amekemea kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa nchi nzima na baadhi ya vyama vya siasa na kupewa jina la ‘OPARESHENI’ ambapo amedai kuwa huu si wakati wa vyama kuanza kampeni, hivyo chama chochote kitakachoendelea na kampeni kwa mtindo huo kuanzia sasa kitachukuliwa hatua kali ikiwemo kukifutia usajili.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat