WAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Morogoro, jioni hii wameandamana kwa amani kutoka maeneo ya Nane Nane walipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche hadi ofisi za makao makuu ya chama hicho ya mkoani hapa, yaliyopo mtaa wa Kingo. Baada ya kufika kwenye ofisi hizo, Heche alizungumza na wafuasi wa chama hicho.
(PICHA ZOTE NA DUNSTAN SHEKIDELE / GPL)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!