StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 1, 2012

DUH, SAKATA LA UMRI WA LULU UTATA MTUPU....

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 


SAKATA la umri wa msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, sasa limepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Septemba 17, 2012.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu, Sinza jijini Dar es Salaam.




Habari zilizopatikana kutoka mahakamani hapo na kuthibitishwa na mmoja wa mawakili wa msaniii huyo, zinaeleza kuwa , shauri hilo litasikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ambao ni January Msoffe, Bernard Luanda na Katherine Oriyo.




Mahakama ya Rufani itafanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuona kama ulikuwa ni sahihi, kukubali kufanya uchunguzi wa umri halali wa mshtakiwa huyo, kufuatia maombi yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka.

Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata baada

ya mawakili wanaomtetea kuomba kesi yake isikilizwe katika Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) wakidai kuwa bado ni mtoto.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat