Mkali Lenex akifanya vitu vyake jukwaani, hakika Serengeti Fiesta Iringa ni Bhaaaaass!!
Ni mkali mwingine kutoka jijini Mwanza kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012, Young KIller akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaondelea kutinga hivi sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Ni mkali mwingine kutoka Morogoro kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaonelea kuingia hivi sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mmoja wa wasanii chipukizi aliyeibukia kwenye shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,kutoka Mkoani Mbeya aitwaye Ney Lee pichani akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani usiku huu kwenye uwanja wa Samora,mkoani Iringa ambako hivi sasa kunarindima tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wadau wa Serengeti fiesta Iringa na Dar es Salaam nao wapo hapa Uwanja wa Samora Iringa kupata burudani
Ndani ya uwanja wa Samora Mjini Iringa ndo kwaaaanza kumekucha katika tamasha kubwa na la aina yake ya SERENGETI FIESTA 2012 ambapo linajiachia usiku huu hadi Bhaaaaaass!!
Wameanza kupanda wasanii chipukizi wa mjini Iringa na vitongoji vyake.




0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!