
Nikki Mbishi akishusha mistari yake mbele ya wakazi wa mji wa Tabota.

watu walivyojutokeza wingi kwenye tamasha la Serenegeto Fiesta

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.

Anaitwa Godzilla,Msanii wa hip hop katika muziki wa kizazi kipya,akiangusha mistari iliyowasisimua mashabiki mbalimbali waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.

Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishangwaka vilivyo usiku wa kuamkia leo,tamasha hilo limefanyika jana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel,mkoani humo.

Moja wa zao la Serengeti Fiesta 2012,Supa Nyota Ney Lee akitumbuiza jukwaani.


Msanii Recho akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani akisindikizwa madens wake
Msanii mahri wa muziki wa kizazi kipya,Ben Paul akionesha kipaji chake ch a kuimba.

Palikuwa hapatoshi ndani ya Tabora usiku wa kuamkia leo.

Rich Mavoko akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku

Sir Juma Natura akikamua usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 202
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!