Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Mkazi wa Kijiji cha Ipelo,Kata ya Kandete Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, Mwalisu Kilole (67) amefariki dunia akiwa shambani kwake baada ya mwili wake kuteketea kwa moto.
Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 5 mwaka huu majira ya saa 1 usiku wakati marehemu huyo akiwa shambani kwake alipokwenda kulima.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Yuda Mwasambogole,amesema kuwa alipata taarifa za kifo cha mtu huyo ambapo alipofuatilia alikuta mwili wa marehemu umeteketea kwa moto na mpaka sasa chanzo cha moto huo hakichaweza kufahamika.
Baada ya uchunguzi kufanywa na madaktari, mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko.Wakati huohuo Mkazi wa Kijiji cha Ifuko Sifa Pascal Nyerenga amefariki dunia baada ya kutumbukia katika Mto Songwe,Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wakati akiogelea.
Marehemu amesadikika kuwa kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kifafa,ambapo mwili wake ulipatika majira ya tatu asubuhi Septemba 5 mwaka huu.
September 8, 2012
MASKINI WEEEEE......AFA KIFO CHA KIKATILI SHAMBANI
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!