StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 15, 2012

GARI LA POLISI LAUA LIKISAFIRISHA MAITI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends  

WATU TISA wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti ya ajali ya barabarani yaliyohusisha Landrover ya polisi iliyokuwa inasafirisha maiti kwenda Musoma na Fuso moja iliyokuwa inakwenda mnadani Singida vijijini.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa mkoa, Linus Sinzumwa, ajali zote mbili zilitokea jana kati ya saa 5:30 asubuhi na 6:30 mchana.

Landrover hiyo mali ya polisi Morogoro ilikuwa na abiria 11 ambao walikuwa wanasindikiza mwili wa askari polisi Regu Kamamo kuupeleka Musoma kwa mazishi.

Kamanda Sinzumwa, alisema kuwa gari la polisi lilipata ajali katika eneo la Manguajunki, nje kidogo ya mji wa Singida katika barabara kuu ya Singida – Mwanza.

Aliwataja waliokufa kwenye ajali ya Landrover kuwa ni, Rosemary Nyabuzuki ambaye ni askari mwenye cheo cha Sajini, Nyamwenda Juma, Rehema Juma na mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Juma.

Kamanda Sinzuma alisema kuwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali zote mbili ingawa alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha huenda ni mwendo mkali.

Katika tukio la pili,Kamanda huyo alisema kuwa Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 126 AEU lililokuwa limepakia wafanyabishara wa minada kutoka Singida mjini kwenda mnada wa Mtavira kata ya Minyughe wilaya ya Singida, lilipinduka na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo na kujeruhi abiria 14.

Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida, Dk Joseph Malunda, aliwataja waliofariki dunia papo hapo kuwa ni Sarafina Ally, Pili Saidi, Charles Thomas na watu wengine wawili waliofahamika kwa jina moja moja la Bakari na Bilali.

Alieleza kuwa hali za majeruhi waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri na kuongeza kuwa maiti zote tisa zimehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa,zikisubiri ndugu zao kuja kuzitambua.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat