StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 15, 2012

LIGI KUU KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Kikosi cha African Lyon 

MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara kwa mwaka 2012/13 unaanza kutimua vumbi leo, ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa nyumbani kucheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pazia la msimu mpya wa ligi hiyo lilifunguliwa rasmi Jumanne wiki hii kwa mechi ya Ngao ya Jamii baina ya bingwa mtetezi na mshindi wa pili wa ligi hiyo kwa msimu uliopita timu ya Azam.

Na katika mchezo huo, Simba iliifunga Azam mabao 3-2 na kunyakua Ngao hiyo. Kwa upande wao Yanga, watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya kucheza na timu iliyopanda daraja msimu huu ya Tanzania Prisons.

Huko kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, timu ya Coastal Union ikicheza na timu ngeni kwenye ligi hiyo ya Mgambo Shooting pia kutoka mkoani humo.

Mechi hiyo nayo inatarajiwa kuwa na uhondo wa aina yake kwani inakutanisha timu mbili kutoka mkoa huo kwenye Ligi Kuu.

Mara ya mwisho kwa timu mbili kukutana na kwenye ligi hiyo ilikuwa kwenye miaka ya 1990 wakati African Sport na Coastal Union zikiwa bado hazijashuka daraja.

Mechi nyingine ni Polisi Morogoro iliyopanda daraja msimu huu itawakaribisha ndugu zake Mtibwa Sugar pia ya Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Wao JKT Ruvu itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi Kibaha, Pwani, Toto African wataikaribisha JKT Oljoro kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Azam itakuwa wageni wa Kagera Sugar mjini Bukoba.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat