Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Arbogast Kiwale kwa pamoja na Balozi wa Japan
Nchini Tanzania ,Masaki Okada wakitia saini mkataba wa kusaidia Ujenzi wa Mabweni mawili ya shule ya sekondari ya kutwa ya wasichana Nachingwea wenye thamani ya dola za marekani 122,333...Mkataba huo
umesainiwa mbele ya Wabunge wa mkoa wa Lindi,Wakuu wa wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri huku Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Katibu Tawala mkoa akishuhudia
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkowe wilayani Ruangwa mwl Shannel Nchimbi akikabidhi hati ya makubaliano ya msaada wa mabweni 2 kwa shule hiyo kwa Balozi wa Japan,Masaki Okada hii katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Wabunge wa Mkoa wa Lindi nao wakishuhudia kuwekwa kwa saini mikataba ya Kusaidia ujenzi wa Mabweni 2 ya shule ya sekondari ya Nkowe wilayani Ruangwa Pamoja na Mabweni mawili ya Shule ya kutwa ya wasichana Nachingwea
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Lindi wakishuhudia tukio hilo la msaada wa kuinua kiwango cha elimu
Picha ya pamoja baada ya kusainiwa mikataba hiyo. Serikali ya Japan imetoa Jumla ya dola za kimarekani 243,698 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni 4 kwa shule za sekondari za Nkowe wilayani Ruangwa Na Shule ya kutwa ya Wasichana wilayani Nachingwea Hatua hiyo imekuja katika jitihada za Nchi ya Japan kukuza Ushirikiano na Tanzania Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada amelala wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ambapo leo atatembelea shule ya sekondari NKOWE na Baadae kuelekea Wilayani Nachingwea. Picha na Habari toka kwa Mdau Abdulaziz video rec,Ruangwa
September 14, 2012
JAPANI YASAIDIA UJENZI WA MABWENI 4 WILAYA ZA NACHINGWEA NA RUANGWA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!