StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 11, 2012

MHESHIMIWA RAIS KIKWETE AFANYA UFUNGUZI WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Nyuma yao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha anayefuatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala Septemba 10, 2012 baada ya kumkabidhi mfano wa funguo kama ishara ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) kilichoko Kunduchi jijini Dar es salaam, pamoja na kuzindua kozi ya kwanza ya mwaka mmoja. Walioketi karibu yake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanachuo wa kozi ya kwanza ya mwaka mmoja katika Chuo cha UIinzi (National Defence College) alichofungua rasmi Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam.(PICHA NA IKULU).

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat