Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa Safari zitazoanzia Station ya Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi. Majaribia hayo yameongozwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba(Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya ukarabati wa njia,injini na mabehewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(Mb),akipanda treni wakati wa majaribio ya Mabehewa sita ya treni kati ya mabehewa kumi na mbili yanatogemewa kutumika na Shirika la reli Tanzania(TRL). Treni hizo zitakayofanya safari zake kutoka Station Dar es Salaam mpaka Ubungo,mapema mwezi wa Kumi.
Baadhi ya wananchi wakipanda katika behewa moja kati ya Sita yaliyofanyiwa majaribio mapema leo kutokea Station mpaka Ubungo(km 12).
Mchuma huo unaondoka
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL) wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi.
Abiria wa majaribio
September 11, 2012
TRENI YA KWANZA YA DAR-UBUNGO YAFANYIWA MAJARIBIO
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!