StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 3, 2012

MWANAMKE AJIFUNGUA KICHAKANI BAADA YA SENSA KUFUNGA ZAHANATI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Mkazi wa kijiji cha Litou wilaya ya Liwale  Nuru Mohamedi Kipeleka (34),amejifungua kichakani  baada ya zahanati kufungwa kutokana na  wahudumu  wa zahanati hiyo  kuteuliwa kuwa  makarahani wa sensa.

Tukio hilo lilitokea jana wakati  Kipeleka  alipopatwa  uchungu na familia yake kuchukua uamuzi wa kumpeleka  kwenye zahanati  ya kijiji ya Kiangara.

Akizungumza na gazeti hili baba wa binti huyo Mohamedi Kipeleka, alisema sababu zilizopelekea  mtoto wake  kujifungua njiani, ni kukosekana kwa mganga kwenye kwenye zahanati  hiyo baada ya wahudumu  wa afya kuteuliwa kuwa makarani wa sensa.

Kipeleka alisema baada ya kufika kwenye zahanati hiyo alikuta imefungwa , na alipouliza wakazi wa maeneo hayo aliambiwa  waganga wamekwenda kwenye zoezi la sensa mtaani.

Alisema baada ya kukuta zahanati imefungwa walilazimika kurudi nyumbani ndipo mwanae alipopatwa na uchungu  na kujifungulia kichakani.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Mtepeka  alikanusha kuwepo kwa tatizo hilo, na kwamba zahanati iko wazi na inawahudumu ambao ni, Abasi Makanga,Abdallaa Likiwa na Aberamani Kenyu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Sensa wilaya ya Liwale Alfredy Mmbaga, alikanusha kusikia tukio hilo, na kuongeza kwamba hajui kama kuna vituo vya afya na zahanati vilivyofungwa  kwa sababu ya waganga wake kuteuliwa kuwa makarani wa sensa wilayani humo.

“Taarifa hii ni  mpya kwangu kwani ndiyo kwanza naipata kwako, hivyo  siwezi kuzungumza chochote” Alisema Mmbaga. 


CHANZO: MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat