VIMWANA 15 wa Redd's Miss Temeke, ambao wameanza rasmi kambi yao katika Club ya TCC Chang'ombe tayari wa kinyang'anyiro cha kanda hiyo, jana safu ya wakufunzi imeongezewa nguvu baada ya Top Model, Leyla Bhanji naye kuanza kuwafunda.
Warembo hao ambao wameanza programu ya shoo kwa wiki iliyopita, chini ya ukufunzi wa Dickson Daud kutoka kikundi cha THT, ambapo ilikuwa ni wiki ya kujiweka sawa zaidi kwa shoo ya ufunguzi ambayo itakuwa tofauti sana kiuchezaji wake, kuwa imezingatia urembo zaidi na umri wa warembo katika utumiaji wa jukwaa.
Warembo hao wanaotoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012, Ijumaa iliyopita wote walipata fursa ya kuangalia shoo iliyofana ya Redd's Miss Ilala katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.
Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Kampuni ya GlobalPublishers kupitia magazeti yake pendwa na Website yao, Dodoma Wine, gazeti la Jambo Leo, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Times FM.
Warembo wanaendelea na mazoezi na leo, na Miss Tanzania anayeshikilia taji hilo, Salha Israel anatarajiwa kuwatembelea Jumatano na hii pia itakuwa ni wiki ya kutembelewa na warembo mbalimbali waliofanikiwa katika fani hiyo katika kuwapa uzoefu wao katika mashindano ya urembo.

0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!