StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 7, 2012

UCC KUZIFUNGIA SIMU ZOTE BANDIA KUANZIA NOVEMBA 2012

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
The IMEI is a unique 15-digit code that identifies a phone. It stands for International Mobile Equipment Identity (IMEI).
IMEI ni namba ya kipekee yenye tarakimu 15 ambayo huonesha utambulisho wa simu. Inatambulika kwa lugha ya kiingereza kama International Mobile Equipment Identity (IMEI).

Kufungiwa kwa simu hizo kutawaathiri tu watumiaji wapya wa vifaa hivi vya mawasiliano vinavyoaminika kuwa bandia.

Mtu yeyote ambaye atanunua bidhaa bandia, hasa simu baada ya Oktoba wanapaswa kufikiri mara mbili kwasababu yupo katika hatari ya kunyimwa haki ya kujiunga na mtandao wowote, Tume ya Mawasiliano ya Uganda imesema. UCC imetoa taarifa hiyo katika vyombo vya habari jana Jumatano kwamba watakuja kufanya hivyo kitaalam na baada ya hapo haitowezekana kwa simu za bandia kutumika kwenye mtandao iliyopo nchini humo ya mawasiliano ya simu kama hatua ya kusimamisha uagizaji wa vifaa feki ambao soko lake limeshamiri nchini humo.
Miezi iliyopita, Tume ya Mawasiliano ya Kenya iliagiza mitandao ya simu nchini humo kuzima sim-cards zote zinazotumiwa katika simu bandia kwenye mitandao yao katika jaribio la kuzuia mauzo ya simu hizo bandia.
Lakini tofauti na Kenya ambayo imeshaanza tayari kazi ya kuzifungia sim-cards katika simu zote bandia na pia kuzuia simu zote mpya za bandia kuweza kupata mitandao, UCC, kulingana na mtendaji mkurugenzi wake Godfrey Mutabazi, itaanza kwa kuzuia simu zote  mpya za bandia kuweza kupata mawasiliano.
"Utitiri wa ghafla wa simu na vifaa vingine bandia vya mawasiliano ya simu ni tatizo kubwa. Vifaa hivyo vipo chini sana katika ubora na wala haviwezi kukidhi viwango vya usalama, na katika hali tofauti tofauti, mionzi kutoka kwenye simu hizo ni zaidi ya kiwango halali na inaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya Waganda. "
Tunaposema simu ni bandia tunamaanisha IMEI yake haitambuliki, haijasajiliwa au haipo katika database ya mtengezaji halali anayezalisha simu yenye nembo husika.
Hata hivyo, Bw. Mutabazi alionya  juu ya hatari ya afya kwamba watumiaji wa bidhaa bandia ni wazi, simu hizo licha ya kuhatarisha afya zao lakini pia ni tishio kwa uchumi wa taifa na usalama.
Kulingana na Mamlaka ya Mapato Uganda, Uganda imeingiza kiasi cha simu zipatazo 120,258 na zinakadiriwa kuwa na thamani ya Shs5.87b kwa mwezi Julai 2012 peke yake, ikilinganishwa na simu 81,650 zilizoingizwa mwezi Mei 2012, ikikadiriwa kuwa na thamani ya Shs3.87b.
(KUTOKANA NA HABARI HII NAHISI PIA TANZANIA ITAFIKA BAADA YA MUDA FLAN, SO CHAKUFANYA ACHA NITAFUTE NAMNA NIUZE MCHINA WANGU KABLA SIJABAMBWA HEHEHE, NAJUA WENZANGU NA MIMI HABARI HII ITAKUWA MSIBA MZITO!)

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat