Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Redds Miss Lake zone 2012/13 Eugene Fabian (katikati) akiwa pamoja na ,
mshindi wa Tatu Happiness Rweyemamu na Kulia kwake ni mshindi wa pili
Happiness Daniel warembo hawa wataingia kambi ya REDDS Miss Tanzania
2012.
******
Jumla ya warembo 30 wanataraji kuingia kambi ya
REDDS MISS TANZANIA 2012 wakati wowote baada ya kumalizika kwa
mashindano ya Vitongoji, Mikoa, na hatimaye Kanda mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Kwa mujibu wa mashindano hayo ya Kanda
ambayo kila Kanda imetoa washindi wa tatu ambao wataziwakilisha Kanda
zaoi katika Shindano hilo kubwa na laiana yake.
Warembo
hao na Kanda zao wanazotoka ni Redds Miss Kanda ya Kaskazini Warida
Frenk, Anande Raziel na Lucy Stefano, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki
2012 ni Rose Lucas, Irine Veda na Joyce Baluhi , Redds Miss Kinondoni
Brigit Alfred, Diana George Hussein na Irene David.
Kanda
nyingine ni Redds Miss Lake zone 2012 Eugene Fabian,Happiness Daniel na
Happiness Rweyemamu, Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester, Flavian
Maeda na Catherine Masumbigana, Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo,
Lightness Michael na Elizabeth Diamond.
Washiriki
wengine watakao ingia Kambini ni kutoka kanda ya Redds Miss Ilala 2012,
Mary Chizi, Magdalena Munisi na Noela Michael, Redds Kanda Vyuo vya
Elimu ya Juu, Virginia Mokiri, Fatma Ramadhani na Fina Revocatus, kanda
nyingine ni ya Kutoka Chuo Kikuu Huria ni Zuwena Nassibu na Redds Miss
Southern Zone Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward.
Kesho Septemba 26, 2012 Kamati ya Miss Tanzaniaikiongozwa na Mkurugenzi
wake Hashim Lundenga kutoka Lino International Agency watakutana na
waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maeleo majira ya
saa 4:00 asubuhi kuzungumzia maandalizi ya Kambi hiyo.
Redds Miss kanda ya Kaskazini Warida Frenk katikati akiwa na washindi
wenzake Anande Raziel kulia na lucy stefano kushoto mara baada ya
kutawazwa kuwa washindi wa Redds Miss Kanda ya kaskazini,Washindi hao
wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya Redds Miss Tanzania hapo baadae
ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds Miss Tanzania.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono
kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa
tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa
shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1,
mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss
Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia
mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana,
kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene
David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irine
akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.
Malkia wa Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester (katikati), akiwa na
mshindi wa pili Flavian Maeda (kushoto), pamoja na Catherine Masumbigana
aliyeshika nafasi ya tatu katika kilele cha mashindano hayo, Ukumbi wa
PTA Sabasaba, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward
Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo (katikati) akiwa na mshindi wa
pili Lightness Michael (kushoto) na mrembo aliyetwaa nafasi ya tatu
Elizabeth Diamond baada ya kumalizika kwa shindano hilo mjini Dodoma
hivi karibuni. warembo hawa wote wameingia kambi ya Miss Tanzania 2012.
Redds Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalena
Munisi (kulia) na mshindi wa tatu Mary Chizi (kushoto) mara baada ya
kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Ilala 2012.
September 25, 2012
WAREMBO WALIOFUZU KUINGIA REDDS MISS TZ NDIO HAWA HAPA
Millionfortune.com
BURUDANI
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!