Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Meli ya Uholanzi inayojulikana kwa jina la ‘Abortion Ship’ imezuiliwa na Jeshi la majini la Morocco kuingia katika mji wa Smir kuelekea bandari ya Morocco.
Meli hiyo inamilikiwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Uholanzi ijulikanayo kama Women on Waves, na kwa sasa eneo la bandari ambalo meli hiyo imezuiliwa limezungukwa na ulinzi mkubwa wa askari.
‘Abortion ship’ imekwenda nchini humo kwa lengo la kuhamasisha utoaji mimba salama kwa wanawake wa Morocco ikiwa ni safari yake ya kwanza katika nchi ya kiislamu.
Utoaji mimba ni kitendo kisichokubalika kisheria nchini Morocco isipokuwa katika mazingira maalumu.
Tayari chombo hicho kimeshasafiri katika nchi kadhaa zinazofuata imani ya dini ya kikristo dhehebu la katoliki zikiwemo Uhispania, Ureno na Ireland.
October 5, 2012
HII NDIO MELI YA UHOLANZI INAYOITWA ‘ABORTION SHIP’
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!