Mashujaa wa Mau Mau
Mahakama kuu nchini Uingereza leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake katika kesi iliyowasilishwa na mashujaa watatu waliopigania uhuru nchini Kenya ,Mau Mau, dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Wakenya hao wanadai waliteswa na kudhulumiwa na serikali ya ukoloni ya Uingereza katika miaka ya 1950, wakati wa harakati za kupigania uhuru wa taifa hilo.
Mnamo mwezi Julai, serikali ya Uingereza ilikiri kwa mara ya kwanza kwamba washukiwa wa vita vya Mau Mau waliteswa na hivyo Uingereza ikaomba radhi.
Mahakama hata hivyo itaamua ikiwa kesi itaendelea au iamrishe walipwe fidia.
Lakini mawakili wa serikali watakuwa wanateta wakisema kuwa kesi ya haki haiwezi kutendeka kwa sababu matukio hayo yalitokea miaka ya hamsini.
Mapema mwaka huu, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Askofu mkuu mstaafu Desmond Tutu, alimtumia ujumbe waziri mkuu David Cameron akimtuhumu kwa kujaribu kukwepa kuwajibika kisheria kwa makosa yaliyofanywa na wakoloni.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!