Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Ujumbe Wenyewe ndio Huu.
Ujumbe ulioachwa na Oscar John (24) mkazi wa mkoa wa Dodoma aliyejinyonga hadi kufa baada ya kuhisi amemuuwa mchumba wake kwa kumkata kata kwa kisu,umepatikana.
Oscar alijinyonga chumbani kwa mchumba wake Maria Chilinde (25) ambaye ni mfanyakazi wa chuo cha VETA mjini Singida baada ya kumkata kata kwa kutumia kisu.
Katika ujumbe huo, marehemu Oscar aliandika ‘mimi Oscar John nimekufa pamoja na Maria,hela elfu tisini pamoja na simu zangu watachukua wazazi wangu.By by wapendwa wote’.
Kwa mujibu wa mkuu wa chuo cha VETA mjini Singida Afridon Mukhomoi, marehemu Oscar atakuwa ameandika ujumbe huo baada ya kubaini amemuuwa Maria na alipomaliza kuuandika, alijitundika kwenye kenchi kwa kutumia pazia na kusababisha kifo chake.
Amesema kuwa wakati tukio hilo la kusikitisha linatokea, yeye hakuwepo lakini alielezwa kuwa baada ya Maria kuzirai na Oscar kuhisi kuwa amefariki dunia, alimfunika kwa shuka na kuandika ujumbe huo na
Marehemu Oscar inadaiwa amefanya unyama huo baada ya wazazi wa Maria kudai mahari ya shilingi milioni mbili,ndipo aolewe na Oscar.Oscar alishindwa kumudu kiwango hicho na hivyo kuamua wote wafe.
October 16, 2012
HUU NDIO UJUMBE ALIOCHA MKAZI MMOJA WA DODOMA KABLA YA KUJINYONGA BAADA YA KUHISI KAMUUA MCHUMBA WAKE.
Millionfortune.com
JAMII
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!