Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
AJALI za barabarani zimeendelea kuutikisa Mkoa wa Kilimanjaro, jana basi
dogo la abiria liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu
watano papo hapo na kujeruhi 13.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Ramadhan Ng’azi, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 1:00
usiku wakati basi hilo likitokea Kijiji cha Ng’uni kwenda Bomang’ombe,
kupitia Kware wilayani Hai.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Mbosho,
Kata ya Masama, baada ya dereva wa basi hilo dogo aina ya Toyota Hiace
namba T179 AAX ambaye hajafahamika, kushindwa kudhibiti gari hilo.
Ng’azi
alisema waliokufa wametambuliwa kuwa ni Elinawenga Leama (90) mkazi wa
Isuka, Fred Jackson (23) mkazi wa Masama na Raphael Kimaro(55) mkazi wa
Ng’uni.
Wengine waliokufa ni Richard Munuo (55) mkazi wa Kijiji cha Ng’uni na Baraka Ng’oko (45), ambaye ni mkazi wa Arusha.
Waliojeruhiwa
na umri wao ukiwa kwenye mabano, ni Oscar Siao (40-45), Alisenda Sirael
(50), Leonard Munisi (32), Hussein Abdi (63), Aminadabu Munuo(6) na
Richard Arnold (18).
Wengine waliojeruhiwa ni David Joshua (39),
Noel Onesmo (25), Marry Witness (44), Walter Tarimo (37), Onisael
Anankya (70), Helea Ngunda (60) na Wilinanda Amosi (37).
Alisema
miili ya marehemu imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali
ya Kibong’oto ,wakati majeruhi walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC
kwa matibabu.
Kaimu kamanda huyo alisema ingawa uchunguzi wa
chanzo cha ajali hiyo unaendelea, lakini inaonyesha mwendokasi
umechangia kwa kiwango kikubwa.
June 19, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!