KESI inayo mkabili
msanii wa Filam nchini Elizabeth Michael (Lulu) imezidi kuwa ngumu baada ya
mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kushindwa kusikiliza Shauri la Umri wa
msanii huyo.
Elizabeth Michael
(Lulu) (aliye vaa kiraia) akirudishwa katika basi la Magereza mara baada ya
kutoka kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili kwenye Mahakama kuu ya Tanzania
kanda ya Dar es Salaam.
Aidha katika kesi
hiyo Kaganda alidai kuwa wamekata rufaa mahakama ya rufaa kupinga mahakama kuu
kusikiliza shauri hilo kutokana na mahakama ya Kisutu kufanya makosa ya
kulipeleka shauri hilo mahakama kuu ambayo haina haki ya kusikiliza shauri hilo
na kutaka lirudishwe tena mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mawakili wanaomtetea
msanii huyo walipinga vikali kauli hiyo nakudai haikufuata taratibu za kisheria
kwa sababu siku ya leo ilikua ni siku ya kusikiliza shauri kuhusu umri na sio
kuleta pingamizi hilo, pamoja na hilo jaji anaesikiliza kesi hiyo hana taarifa
zozote kuhusiana na jambo hilo na kulifanya likose uhalali wa kukubalika.
Hata hivyo jaji Mkuu
anae sikiliza Shauri hiolo Dk.Twalibu Fauzi, alikataa katakata maelezo ya
wakili wa upande wa Serikali nakusema suala hilo aliwezi kurudishwa tena
Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu na kutoa kauli kwamba Mahakama Kuu itaanza
kusikiliza kesi hiyo July 9 mwaka huu. Lulu amerejeshwa Rumande kuendelea
kusubiri hatima ya maamuzi ya kisheria.
