Meneja
Uhusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania, Jackson Mmbando
akimkabidhi Jamila Juma simu ya mkononi aina ya Sumsung, baada kuibuka mshindi
kwa kuichambua vyema huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
Pichani
(kushoto) wakazi wa Mwanza, Jamila Juma na Sandra Mwashitete wakipewa maelekezo
mafupi namna ya kutumia mtandao wa Airtel pamoja na huduma zake mbalimbali,
mara baada ya kujishindia simu aina ya Sumsung, wakati kampuni ya Airtel
ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5, iliofanyika
jana kwenye viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza.
Ni
Mzee wa Makamo hivi lakini alionesha umahiri wake mkubwa wa kuwachangamsha
vilivyo wakazi wa jiji la Mwanza. Anaitwa Mzee Salum akikamua jukwaani jana
kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya
ya Airtel Jiunge na Supa5.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiendelea kuhamia
Airtel na kupata huduma mbalimbali za kampuni hiyo, jana jioni kwenye viwanja
vya Furahisha wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na
Supa5.
Baadhi
ya wasanii wa kikundi cha Kinonko chenye maskani yake pale Kinondoni,
kikionesha umahiri wake wa kucheza mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la
Mwanza waliojitokeza kwenye viwanja vya Furahisha wakati wa uzinduzi rasmi wa
huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
Sehemu
ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye uzinduzi
rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5, uliofanyika kwenye viwanja vya
Furahisha jijini humo.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya na kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi kutoka
Temeke, jijini Dar, Juma Nature na msanii mwenzake KR-Mulla (pichani juu)
wakilishambulia jukwaa huku shangwe kubwa ikilipuka kutoka kwa sehemu kubwa ya
wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma
mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHER