Mbunge wa
jimbo la Ubungo John Mnyika ametolewa katika ukumbi wa Bunge la Tanzania mapema jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati
akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu
kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais
Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi
Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa
Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa
bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti
bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka
makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina
mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya
kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti
iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho.
Mh. John Mnyika akichangia bungeni
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!