Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye
maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani leo, waziri
wake anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi amesema
vita dhidi ya dawa za hizo nchini inakwazwa na mkanganyiko wa sheria za
kudhibiti uhalifu huo ambao una athari kubwa kwa nguvukazi ya Taifa.
Lukuvi
alisema juzi mjini Dodoma kuwa mkanganyiko wa sheria unagusa mfumo
mzima wa uchukuaji wa hatua dhidi ya watuhumiwa kuanzia kukamatwa kwao,
maandalizi ya mashitaka husika, kufikishwa mahakamani, vidhibiti
walivyokamatwa navyo na hata hukumu zinazotolewa.
Lukuvi ambaye
alikuwa akizungumzia maadhimisho hayo ambayo kitaifa yanafanyika leo
jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kasoro hizo watuhumiwa wengi
wamekuwa wakiachiwa hata baada ya kufikishwa mahakamani.
Alisema
Serikali iko kwenye maandalizi ya sheria mpya ambayo pamoja na mambo
mengine haitatoa mwanya wa chaguo la hukumu ya faini kwa wale
watakaotiwa hatiani na pia haitatoa mwanya wa kutumiwa kwa sheria
nyingine kwa makosa ya dawa za kulevya.
“Wataalamu wetu
wanatwambia kwamba ziko sheria nyingine kadhaa ambazo zinatumika
kuwashtaki hawa watuhumiwa wa dawa za kulevya, sasa ndiyo maana wakati
mwingine hata hukumu hazisikiki maana watu wanapigwa faini, wanalipa
kisha wanaondoka na kuendelea na biashara hii,”alisema waziri huyo na
kuongeza:
“Na hawa vijana wadogo wanaotumiwa kusafirisha, maana
kazi ya kusafirisha inafanywa na vijana wadogo tu, wakitumwa wala
hawasiti maana wanafahamu kwamba hata wakikamatwa adhabu yao ni faini na
mtu wa kulipa faini yupo”.
Alisema mchakato wa kuuhisha sheria
hiyo ya dawa za kulevya unaendelea na kwamba Serikali itafanya kila
linalowezekana iweze kuwasilishwa bungeni mwaka huu.
Lukuvi
alisema mkanganyiko uliopo umekuwa ukikwaza juhudi za serikali za
kudhinbiti dawa za kulevya na kutoa mfano wa sheria inayolazimisha
kupelekwa madawa ya kulevywa mahakamani kama ushahidi kila wakati hata
kama kesi itachukua muda mrefu.
“Hizi dawa zinabadilika,
mathalan kama wakati mnamkamata mtuhumiwa zilikuwa na uzito kiasi
fulani, kadri zinavyotunzwa uzito unapungua na hata kupata mabadiliko ya
kikemikali, hivyo mabadiliko hayo yanafanya dawa hizi zisifae wakati wa
kuthibitisha ukweli mahakamani,”alisema.
Kutokana na hilo,
alisema ni vigumu kwa binadamu wa kuvumia hadi mwisho kwani wakati
mwingine hujikuta katika majaribu ya ama kuiba madawa hayo au kuyatumi
lakini pia mahakama kukosesha imani kwani vitu vinavyokamatwa
hurudishiwa wahusika wakati sheria inasema vitaifishwe.
“Mfano
mahakama Jijini Dar es Salaam iliamuru kuwa mtambo mkubwa uliokuwa
umekamatwa urudishwe kwa mhusika jambo ambalo ni hatari kubwa,”alisema.
Alisema
vyombo vya sheria ni kama vimekuwa vikikwepa kutumia sheria husika ya
dawa za kulevya inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 au kifungo cha
maisha kwa wanaotiwa hatiani na kwamba sheria mpya itaziba mianya
iliyopo.
“Si kwamba nawalaumu mahakimu na majaji kwani wanatumia
sheria nyingine zilizopo pia hutegemea mashitaka yamefunguliwa kwa
sheria ipi, nakumbuka ni Jaji mmoja tu Nyangarika (Kassim) ambaye
aliwahi kutoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa mkoani
Mtwara, waliobaki ni faini, faini tu,”alisema.
Lukuvi alisema
tatizo la dawa za kulevya nchini bado ni kubwa licha ya juhudi
mbalimbali za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa ambao
wengi wamekuwa wakiachiwa na ama kesi zao kuchukua muda mrefu bila ya
kutolewa hukumu.
Alisema maadhimisho hayo yanafanyika katika
kipindi ambacho kumekuwa na ongezeko kubwa la usafirishaji wa kiasi
kikubwa cha dawa za kulevya nchini hasa za viwandani zikiwemo heroin na
Cocaine.Waziri alitoa mfano kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi
Mei, 2012 kilo 234 za heroin zilikamatwa na kuwa kiasi hicho ni kikubwa
kukamatwa katika kipindi kifupi.
Lukuvi alisema kuwa ongezeko
la dawa za kulevya linaashiria kuwepo ongezeko la matumizi ya dawa hizo
nchini, hali ambayo inatishia ongezeko la maambukuzi ya VVU miongoni mwa
watumiaji wa dawa hizo.
Kwa mujibu wa Lukuvi, kiwango cha
maambuki ya VVU miongoni mwa watumiaji kwa njia ya kujidunga ni asilimia
42 ikiwa ni ytofauti kubwa na kiwango kwa jamii ambacho ni
asilimia2012-06-25 5.8.
Lukuvi ambaye aliongozana na baadhi ya
wanasheria wa kitendo cha madawa ya kulevya, walisema wakati wowote
watatoa pendekezo serikalini kuondoa kigugumizi kwa serikalini ili kila
anayekamatwa na kuthibitika kwa maandishi afungwe mara moja.
SOURCE: MWANANCHI
June 26, 2012
SERIKALI YALIA NA SHERIA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget