Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
WAKATI Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na kati, Cecafa,
likitaraji kuweka hadharani majina ya timu zilizothibitisha ushiriki
wake mwaka huu, Wau Salaam ya Sudan ya Kusini imekuwa ya kwanza
kuthibitisha ushiriki wake.
Wau inashiriki michuano hiyo kwa mara
ya kwanza ikitokea taifa hilo lililopata uhuru wake Septemba 2011 baada
ya kujitenga kutoka Sudan Kaskazini.
Michuano ya Kombe la
Kagame imepangwa kuanza Julai 14 hadi 28 huku timu 12 zikitarajiwa
kushiriki katika mashindano hayo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Katibu
wa Cecafa, Nicholaus Musonye alisema jana kuwa Juni 24 ilikuwa mwisho
wa uthibitisho na leo wataweka rasmi majina ya timu zilizofanikiwa
kuthibitisha kabla ya kupanga ratiba hiyo katika droo itakayofanyika
mwishoni mwa juma hili Jijini Dar es Salaam.
Musonye alisema
mpaka sasa maandalizi yanakwenda vyema huku akiomba wadau wa michezo
kusaidia upatikana wa fedha kwa ajili ya timu shiriki ili michuano hiyo
ifanyike kwa wakati.
"Tutatangaza timu zote kesho, na timu
waalikwa, kwa sasa maandalizi yanakwenda vizuri na tumekuwa
tukiwasiliana na waandaaji ambao ni TFF nao wanaendelea vizuri.
"Kikubwa
kwa sasa tunaomba misaada kwa wapenzi wa soka kujitokeza katika
kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kwa wakati," alisema Musonye.
Timu
zinazotaraji kushiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Tusker ya
Kenya, URA (Uganda), APR (Rwanda), Coffee (Ethiopia), Elman (Somalia) na
Atletico Olympio ya Burundi.
Nyingine zitakazowania ubingwa
unaoshikiliwa na Yanga ni Wau Salaam (Sudan Kusini), Red Sea (Eritrea)
Al Hilal (Sudan), Mafunzo (Zanzibar) na wenyeji Tanzania
watakaowakilishwa na timu za Simba na Azam.
June 26, 2012
WAU SALAAM YA SUDAN KUSINI YA KWANZA KUTHIBITISHA KAGAME CUP
Millionfortune.com
MICHEZO
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget