StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

June 26, 2012

SIMBA WAMKATIA TAMAA YONDANI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

WAKATI mwenyekiti wa Simba, Ismail aden Rage akijigamba kulijumuisha jina la mchezaji Kelvin Yondani katika usajili, habari ambazo millionfortune.com imezipata, ni kwamba klabu hiyo imeamua kuachana na mchezaji huyo.

Simba ilikuwa ikihaha kumnusuru beki huyo ambaye amekwishajichomoza Yanga na hata kuanza mazoezi wakitaka kumrejeshea fedha zake apeleke Yanga na arudi kundini.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya  Yondan kuanza mazoezi Yanga, na viongozi na wadau wakubwa wa Simba walikuwa katika hekaheka za kumrudisha kundini.

Awali Habari ambazo Mwananchi ilizipata zilidai kuwa mdau mmoja wa Simba alikutana na wadau na viongozi wa Simba pamoja na Yondani mwenyewe wakimshawisi wampatie fedha, kiasi alichochukua ili azirejeshe Yanga.

Chanzo cha habari kinasema kuwa wadau na wapenzi wa Simba hawakuridhishwa na hatua ya beki huyo kwenda Yanga na kwamba anahitajika kwa kiasi kikubwa Simba.

Baada ya Yondani kuonyesha kuanza mapenzi mapya na Yanga, watu wa karibu wa Simba wamepitisha azimia la kuachana na beki huyo huku wakiamini kuwa wachezaji waliopo wanaweza kuvaa viatu vyake.

"Tumeamua kuachana na Yondani baada ya kumuona Lino Musonda, anacheza vizuri beki wa kati na tunaamini atatusaidia," kilipasha chanzo hicho.

Kiliendelea kudai chanzo hicho kuwa, wasiwasi mkubwa ulikuwa beki wa kati lakini baada ya kupatikana Musonda, kwa pamoja waliridhia beki huyo aende akacheze soka Yanga.

Wakati hayo yakijiri jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa na Mwananchi Jumapili akikazia kusema Yondani amekwenda Yanga kutia mashamsham ya mazoezi lakini bado ni mchezaji wao halali.

"Yanga wanajifurahisha wenyewe na kelele zao kamwe hazinitishi...mimi nasema mbivu na mbichi vitajulikana Juni 30 tutakapoweka hadharani kikosi chetu kitakashiriki Ligi Kuu msimu ujao," alisema Rage.

Katika hatua nyingine, kocha wa Simba, Milovan Cirkovic aliyewasili jijini Dar es Salaam juzi usiku akitokea Serbia alikokuwa kwa mapuziko, anatarajia kuanza mikakati yake leo ya kuinoa Simba kwa Michuano ya Kagame iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Julai 14 mwaka huu.

Kocha huyo pia ataitumia nafasi hiyo kuangalia uwezo wa wachezaji wapya wa kikosi hicho ambao walisajiliwa na  hivi karibuni bila ya yeye kuwepo licha ya uongozi wa kilabu hiyo kudai kuwa ulikuwa umepata baraka zake zote.

Kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu ambacho kilikuwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Kagame.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa timu hiyo haina muda wa kupoteza kwa sasa na leo jioni itaendelea na mzoezi yake kwenye Viwanja vya Klabu ya Sigara, TCC, Chang’ombe, Dar es Salaam.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat