Meneja
wa bia ya Serengeti lager Bw. Allan Chonjo (katikati) akizumgumza na
waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa wanne wa Bajaj,
pikipiki, Jenereta katika droo ya tisa ya promsheni ya VUMBUA HAZINA
CHINI YA KIZIBO na SBL, inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti
hapa nchini. kulia ni Meneja Mawasilino wa SBL,Mwakilishi kutoka bodi
ya bahati nasibu ya taifa Bw.Bakari Maggid na shoto kabisa ni
Muwakilishi wa kampuni ya PWC,Bwa.Tumainieli Marisa wakishuhudia tukio
hilo.
**********
WASHINDI
WENGINE WANNE WASHINDA ZAWADI ZA SBL,WAWILI WASHINDA GENERETA, MMOJA
AJISHINDIA PIKIPIKI,HUKU MWINGINE AKIJINYAKULIA BAJAJ, ZAWADI ZOTE MPYA
KABISA,
Ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL.
July3,2012,
Dar Es Salaam:Kampuni ya bia ya Serengeti leo imeendelea na droo ya
tisa katika promosheni inayoendelea ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’
iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo SBL zilizopo maeneo ya
Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi
kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya
kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH
MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium
Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hiyo nchi
nzima ambapo kwa mara nyingine washindi wane wameweza kuibuka na ushindi
katika droo iliyochezeshwa leo asubuhi.
Akiongea
na wandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo hiyo, meneja wa bia ya
serengeti lager bw. Allan Chonjo amesema “ni wiki ya tisa sasa ambapo
tunaendelea na promosheni yetu ambayo bila shaka watanzania wengi
mmekuwa mkishuhudia watanzania wenzenu wakijishindia zawadi mbalimbali
nakukabidhiwa pale walipojipatia zawadi hizo’ naendelewa kuwasisitiza
wateja wetu na watatnzania wote kwa ujumla kuwa bado zawadi zipo nyingi
na kwambakila mmoja wenu anaweza kushinda kama vile ambavyo wengine
wanajishinadia.
Washindi
wetu katika droo hii ya tisa ni bwana Boaz Mtukula kutoka Mwanza
ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Twiga Bancorp mywaji wa bia ya Tusker
Lager na bwana Richard Valerian kutoka Dar Es Salaam anayefanya kazi
Bandarini mywaji wa Tusker pia ambao wote kwa pamoja wamejishindia
jenereta mpya kabisa, na bibi Rahma Ally mkazi wa Temeke jijini Dar Es
Salaam ambaye amejinyakulia pikipiki mpya mywaji wa bia ya Serengeti
Premium Lager na Bwana Richard Mbizi mkazi wa Kimara jijini Dar Es
Salaam amejishindia bajaj mpya kabisa, zawadi zote kutoka SBL.
CHANZO: FATHER KIDEVU