Haya ndio Magari Mawili aina ya 'VOLKS WAGON AMAROK' yaliyonunuliwa na Mfanyabiashara maarufu nchini Said Bhakresa.
Pichani
Juu na Chini ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD
inayouza magari hayo Bw. Julius Guni(kushoto) akimkabidhi Funguo pamoja
na Manual Book za magari hayo mwakilishi wa mzee Bhakresa Bw. Omar Said
kutoka Bhakresa Food Products.
Bw. Omar Said katika pozi baada ya kukabidhiwa rasmi magari hayo.
Bw. Omar Said akichomeka funguo kuwasha moja ya magari hayo.
Mkurugenzi
mpya wa kampuni mpya ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Alfred Minja
akiwajibika ofisini kwake kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na
wateja wanapata taarifa za kutosha kuhusiana na kampuni hiyo pamoja na
magari wanayouza.
Kanpuni
hiyo imeanza kazi rasmi tarehe 1 Julai mwaka huu chini ya Mkurugenzi
huyo mpya na tayari leo tarehe 11 Julai wamefanikiwa kuuza magari mawili
aina ya 'VOLKS WAGON AMAROK'.
Pichani
Juu na Chini ni Fundi wa Kampuni ya Alliance Auto (T) LTD Bw. Dennis
Dismas akifanya Services ya Magari ya Wateja wa Kampuni hiyo kwa
Teknolojia ya kisasa inayotumia Kompyuta.
Mzigo
wa kutosha wa magari aina ya 'VOLKS WAGON AMAROK' katika yadi ya
kampuni ya Alliance Autos (T) LTD iliyopo barabara ya Pugu/Nyerere
jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!