Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
WAZIRI
wa Uchukuzi Dk, Harson Mwakyembe, amesema Oktoba mwaka huu, wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam, wataanza kutumia usafiri wa reli.Mwakyembe
alisema hayo juzi Dar es Salaam baada ya kutembelea Karakana ya Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL), na kukagua maendeleo ya mradi wa usafiri wa
reli ndani ya Jiji.
Katika ziara hiyo, waziri huyo pia aliagiza watu waliojenga ndani ya meta 15 kutoka katikati ya reli kuondoka mara moja.
Waziri
huyo alisema vinginevyo wakati ukifika, nyumba za maeneo hayo
zitavunjwa kwa nguvu na kwamba wamiliki wake hawatalipwa fidia.
“Nikifika
bungeni Dododoma nitalizungumzia suala hili kwa sababu nimeshuhudia
wazi watu wakiwa wanaishi katika maeneo ambayo hayastahili. Wengine
wamefikia hatua ya kulima mazao mbalimbali karibu na reli, jambo ambalo
ni la hatari kwa usalama wao,” alisema.
Alisema tatizo la
msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam litamalizika Oktoba
mwaka huu baada ya kukamilika kwa ukarabari wa mabehewa na reli
kutoka Ubungo Maziwa hadi Stesheni.
Dk Mwakyembe alisema Serikali
imelazimika kutumia fedha za ndani kukarabati mabehewa na reli, ili
kuharakisha mkakati wa kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar
es Salaam.
“Serikali imeamua kufanya matengenezo ya mabehewa
na ukarabati wa reli kuanzia Ubungo Maziwa hadi Stesheni ili kupunguza
kama si kumaliza kabisa tatizo la msongamano wa magari katika Jiji la
Dar es Salaa na kuruhusu shughuli za kiuchumi kuchukua nafasi ,” alisema
Dk Mwakyembe.
Alielezea matumaini yake kuwa kwa kushirikiana
na Wizara ya Ujenzi tatizo la msongamano wa magari litakwisha kabisa
hasa kwa kuzingatia kuwa kuna mradi wa magari yaendayo kasi.
Alisema ingawa Serikali inaendelea na jitihada hizo, lakini inakwazwa na tatizo la kukosekana kwa mali pa kuegeshea magari.
“
Sawa tunafanya jitihaza za kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la
msongamano wa magairi jijini Dar es Salaam, lakini kuna changamoto ya
kukosekana kwa sehemu za kuegesha magari,” alisema.
Na: Mwananchi
July 12, 2012
Usafiri wa treli Dar kuanza Oktoba
Millionfortune.com
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!