Bondia
Japhet Kaseba, akiingia uwanjani huku akiwa ameaongozana na wapambe
wake, baada ya kuitwa kupanda jukwaani tayari kwa pambano lake na
Francis Cheka, pambano lililokuwa lifanyike jana kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Lakini
pambano hilo halikuweza kufanyika baada ya Bondia Francis Cheka, kugoma
kupanda ulingoni kuzichapa na Kaseba, huku akisikika kushikilia msimamo
wake 'eti hawezi kupigana na bondia ambaye hana kiwango wala uwezo wa
kucheza na yeye, na pia bondia ambaye ha rekodi nzuri katika michezo
yake, ambapo alisema kuwa eti amecheza michezo mitatu, amedroo 1,
ameshinda 1 na kupoteza 1, wakati yeye anarekodi nzuri ya kimataifa tena
akiwa amemzidi hadi uzito bondia huyo. ENDELEA KUSOMA PICHA YA PILI.
Hapa
Bondia Kaseba, akiwa katika maandalizi, kabla ya kuitwa kupanda
jukwaani, huku akiwa na usongo wa kukutana na Cheka ili kulipiza kisasi
na kufuta kile kilichoonekana kuzidiwa wakati wa pambano lao la kwanza
lililovinjika mwaka jana katika Uwanja wa Uhuru. ENDELEA KUSOMA PICHA YA
TATU.
Hapa
Cheka, akishaurina jambo na mdogo wake ili kutopanda ulingoni wakati
tayari amekwishaitwa kupanda Ulingoni tayari kwa pambano na Kaseba.
Huwezi
kuamini Bondi huyu, Cheka, hadi dakika ya meisho hakupanda jukwaani
kimchezo, ambpo aliamua kupanda huku akiwa ametinga mavazi yake hivi
hivi kama unavyomuona, huku akiomba apewe Mic ili kuweka wazi jambo
lililomfanya asipande ulingoni, lakini alinyimwa Mic na kuamua kushuka
na kutimka zake.
Ukwweli
wa jambo hilo kama alivyokaririwa Bondia Cheka, ni kwamba, Cheka
alikwisha tangaza toka awali kuwa hatoweza kucheza na Kaseba kwa vigezo
hivyo vilivyokwishatajwa picha ya juu, ambapo alikuwa ameahidiwa
kupiganishwa na Bondia kutoka nchini Malawi, jambo ambalo alikubaliana
nalo na baadaye akabadilishiwa ghafla na kutakiwa kucheza na Kaseba.
Cheka
alisema kuwa, baada ya kueleza hayo aliamua kurejesha fedha na kuweka
msimamo wake wa kutocheza na Kaseba, lakini waandaaji hakutaka kuweka
wazi ambapo waliamua kuwadakisha baadhi ya wananiliu ili kutoandika
ukweli juu ya hili, ili isije bumbuluka na kuharibu utaratibu mzima wa
kurejesha fedha na gharama ambazo tayari zilikwisha tumika. ENDELEA
picha ya chini.
Lakini
Ukweli ulikuwa ukijulikana tangu awali na waandaaji walikuwa wakijua
kila kitu, na ndiyo maana Cheka alionekana akirandaranda tu uwanjani
hapo bila kuchukuliwa hatua, jambo la kushangaza ni kwamba iwapo
waandaaji kweli walimsainisha mkataba na kumlipa fedha kwa ajili ya
kucheza na alifika uwanjani hapo na kugoma kupanda ulingoni, ilikuwaje
wasimkamate na kumchukulia hatua?? , alipouliza Cheka sababu za kusaini
mkataba na hadi siku moja kabla ya pambano akaonekana akipima uzito na
mpinazni wake, alidai kuwa 'eti' ''kupima uzito na kusaini mkataba si
sababu ila sababu alitaka apewe Mic ili atangaze hadharani lakini
alinyimwa hivyo, ukweli amebakia nao mwenyewe na baadhi ya watu
wanaofahamu, na kuwaomba radhi mashabiki wake kuwa hakukusudia kufanya
hivyo na wala si kumuogopa Kaseba ila ni ubabaishaji wa Waandaaji, ambao
hufanywa ili kuwanufaisha wao tu'' alisema
Cheka akiwasiliana huku akitafuta njia ya kusepa uwajani hapo.
Mashabiki wakimzonga Cheka asitoke uwanjani hapo.
Cheka akitoka kwa mbinde uwanjani hapo.
Mawe, Chupa za maji na mikojo, zilianza kurushwa, akirushiwa Cheka, kama unavyoona wapambe wake wakiwa macho juu kukwepa chupa.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!