StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

July 11, 2012

KONA YA UDAKU: NJEMBA AMKIMBIA DEMU GESTI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



TIMBWILI la aina yake limeibuka baada ya msichana mmoja aliyedaiwa kuwa changudoa kumng’ang’ania njemba moja iliyojulikana kwa jina moja la Shabani kwa madai kwamba alimkimbia gesti bila kumpa fedha yake baada ya kumla uroda.
Tukio hilo la aibu lilitokea Jumamosi, Julai 7, mwaka huu mishale ya saa tisa na dakika zake za usiku, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikipiga shoo.
Dada huyo ambaye alionekana kucharuka vikali, alimtaka jamaa huyo kumpa chake baada ya yeye kumtimizia haja zake.
“Huyu si mstaarabu kabisa...mimi sikubali hadi anipe changu. Nilikuwa naye gesti, akaniambia atanipa pesa yangu kwenye gari, baadaye natoka nje nakuta ameondoka. Anipe 20,000 yangu tuliyokubaliana,” alipiga kelele dada huyo huku waungwana wakijaribu kuwasuluhisha.
Hata hivyo, pamoja na varangati hilo, ‘chips funga’ huyo hakuambulia 20,000 achilia mbali buku mbili.
Mwanaume aliyekuwa akifanyiwa vagi na dada huyo, alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya tukio hilo, hakutoa ushirikiano ambapo alisisitiza picha zilizopigwa zifutwe kabla hajafanya kitu mbaya.
“Brother kwa usalama wako nakuambia futa hizo picha, hunijui mimi ni nani, sasa usitafute matatizo,” alichimba mkwara ambao haukusaidia kitu, ndiyo maana sasa hivi unasoma habari hii na picha za kumwaga ukurasa wa nyuma.

SOURCE: www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat