Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi
akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya
Kata ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika
jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh.
milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi
wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi
wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya
Kinondoni, Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na
Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk.
Wana-CCM Kata ya Kimara wakishangilia wakati wa hafla hiyo.
Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakijimwaya mwaya kucheza muziki
wa taarab, kushangilia makabidhiano ya vifaa hivyo vya huduma na tiba
kwa Zahanati yao.
Baadhi ya wanachama wa Jumuia ya Wazazi waliohudhuria sherehe hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo ya
makabidhiano ya vifaa vya huduma na tiba kwa Zahanati ya Kimara. Kulia
(Mwenye koti) ni Diwani wa Kata hiyo ya Kimara kwa tiketi ya Chadema. Picha na na Bashir Nkoromo
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!