Mkurugenzi wa shindano hilo, Methuselah Magese akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Meneja wa hoteli ya Travertine, Ferdinand Mtweve (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari.
Mamiss wakiwa mbele ya waandishi.
Hapa wakiwa na mwalimu wao Mkude Kilosa wakicheza ngoma za asili mbele ya waandishi.
Miss Utalii Kinondoni mwaka jana, Sofia Dio akiwa na washiriki wa sasa.
Shindano la kumtafuta Miss Utalii Kinondoni linatarajiwa kufanyika Julai 20 mwaka huu katika hoteli ya Travertine jijini Dar ambapo washiriki 13 wataonesha makali yao jukwaani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa shindano hilo Methuselah Magese alisema warembo hao wamekwiva katika kucheza ngoma za asili na mambo mengine mengi ambayo wanafundishwa na walimu mahiri.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!