Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa (kulia)
akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic
Kacou (kushoto) katika banda la mfuko huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel (kulia) akisalmiana na Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou. Katikati ni
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Dkt. Alberic Kacou akitia saini kitabu cha wageni katika banda la mfuko
wa fursa sawa kwa wote (EOTF).
Dkt. Alberic Kacou akitazama Juisi
asilia ambao haijachanganywa na kemikali yoyote zinazotengenezwa na
kikundi cha Wajasiriamali wa KYM'S ENTERPRISES cha Kibaha wanaopatikana
katika banda la mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOSF).
Katika ziara hiyo Dkt. Alberic
Kacou alikutana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda
(Kushoto) alipotembelea banda la mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Tanzania Dkt. Alberic Kacou akitazama chakula cha aina ya Senene
kilichofungashwa na majani maalum ya Mgomba, Chakula hicho ni maarufu
kwa wenyeji wa mkoa wa Kagera.
Afisa Mipango wa (EOTF) Bi. Rehema
Batakanwa(kulia) akitoa maelezo bidhaa za Vitenge vinavyotengenezwa na
Maare Enterprises kwa Dkt. Alberic Kacou (katikati) wakati wa ziara yake
katika Banda la mfuko wa fursa sawa kwa wote (EOTF). Kushoto ni
Mkurugenzi wa Maare Enterprises Bi. Florence Maare.
Dkt. Alberic Kacou akionekana kuvutiwa moja ya bidhaa katika banda hilo.
Meneja Mauzo na Masoko wa Moring
Natural Products Christina Ngoti (kulia) akitolea maelezo ya dawa ya
asili isiyonakemikali aina ya Mlonge inayotibu Mangonjwa 300 kwa Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou (katikati). Kulia
ni Afisa Mipango wa (EOTF) Bi. Rehema Batakanwa.
Dkt. Ableric Kacou (kulia)
akibadilishana mawazo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi
pamoja na Mwenyekiti wa mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) Mama Anna
Mkapa (katikati) wakati alipotembelea banda hilo katika maonyesho ya 36
ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Tanzania Dkt. Alberic Kacou (katikati) akiagana na Mwenyekiti wa mfuko
wa Fursa sawa kwa wote Mama Anna Mkapa baada ya kumaliza kutemebelea
mabanda ya wajasiriamali waliowezeshwa na mfuko huo. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel.