Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lina mpango wa kujenga nyumba 15,000
hadi ifikapo mwaka 2015 na kuziuza kwa bei nafuu kwa wananchi wenye
kipato cha chini.
Mkurungenzi Mkuu wa shirika hilo Nehemiah
Mchechu alisema Jijini Dar es Salaam jana kuwa nyumba hizo zitaanza
kuuzwa kati ya Sh25milioni hadi Sh40 milioni kwa lengo la kumsaidia
mwananchi wa kipato cha chini.
Baada ya kusaini mkopo wa Sh165
bilioni kutoka kwenye Taasisi tisa za kifedha,Mchechu alisema fedha hizi
zitawasaidia katika mradi wa ujenzi wa nyumba na ununuzi wa ardhi ya
akiba katika mikoa mbalimbali nchini.
“Nyumba tulizojenga zaidi
ya 1,500 kwa mwaka huu zimewalenga wananchi wa kipato cha chini yule
ambaye atashindwa kununua nyumba ya Sh70m ataweza kununua nyumba za
bei nafuu ambazo zitauzwa Sh25 hadi 40 milioni”alisema na kuongeza;
“Mradi
huu wa ujenzi umeanza kutekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma
,Arusha na Dodoma huku miradi mingine ipo njiani kutekelezwa” alisema
Mchechu
Pia alisema kati ya fedha hizo zilizotolewa Sh23
bilioni zitapelekwa kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu ambazo nyumba
hizo zitawalenga wananchi wa kipato cha chini.
Kwa upande wake
Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka
alisema wananchi wametakiwa kununua nyumba badala ya kununua viwanja ili
kuepuka gharama zisizokuwa na msingi.
Waziri huyo alisema
wananchi wataweza kukopa nyumba hizo ambazo mikopo yake italipwa kwa
riba ya chini ili waweze kunufaika na mradi huo.
“Wananchi
wanunue nyumba badala ya kununua viwanja, hii itamrahisishia kupunguza
gharama ya kununua kiwanja na kujenga ambayo kiwango chake ni
kikubwa”alisema Profesa Tibaijuka.
Profesa Tibaijuka alisema kati ya nyumba hizo zinazojengwa asilimia 25 zitabaki kwa ajili ya watu ambao watahitaji kupanga.