StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

July 12, 2012

(SAYLA) KUZINDULIWA JIJINI ARUSHA, FILAMU YA KUCHANGIA MATIBABU YA SAJUKI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, akielezea jambo wakati akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam, juu ya uzindi wa Filamu ya SAYLA, filamu ambayo ni muendelezo wa harambee za kumsaidia msanii mwenzao wa filamu hapa nchi Sajuki, filamu ambayo itaazinduliwa katika mikoa minne ya Dodoma, Dar es samaam,Morogoro na Arusha, kulia ni Mke wa Sajuki Wastara Juma" wastara"
*******
 
Tarehe 13 Mwezi wa Saba, 2012 katika jiji la Arusha, filamu ya SAYLA itazinduliwa rasmi. Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii na watu maarufu takribani 27 ilirekodiwa maalum kwa ajili ya kuonyesha kuwa kwa kutumia sanaa, sisi watanzania tunaweza kusaidiana wakati wa matatizo. 

Filamu hii maalum kwa ajili ya kuwasaidia Sajuki na Wastara waliokuwa katika wakati mgumu wa kutafuta pesa za matibabu, itazinduliwa kwenye ukumbi wa Naura Springs na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu nchini akiwemo Mh Shyrose Bhanji na wabunge wengine wa  Bunge la Afrika Mashariki, Wema Sepetu akiongoza kundi la wasanii wa Bongo Movie pamoja na wengine kama Snura, Shilole ambao watatumbuiza kwa kushirikiana na Ndege mnana Linah, kwa mara ya kwanza jijini Arusha toka adondoke.

SAYLA ni filamu ya kihistoria iliyoshirikisha idadi ya kubwa ya mastaa kuliko yeyote ile, itazinduliwa pamoja na video na behind the scene za nyimbo ya Mboni yangu!

Baadhi ya watu walioshiriki kwenye hiyo project ni kama ifuatavyo: Mh Zitto Kabwe, Mh January Makamba, Mh Halima Mdee, Mh Esther Bulaya, Mh Vicky Kamata, Mh Shyrose Bhanji, Mzee Chillo, Mzee Hashim Kambi, Muhogo Mchungu, Bi Kidude, Sharo Milionea, Mboto, Kitale, Wema Sepetu, Davina, Ephrahim Kibonde, Adam Mchomvu, Arnold Kayanda, George Goyayi, Mairmatha wa Jesse, Rose Chitala, Ruben Ndege, Irene Paul, Dully Sykes, Chege, Madee, Recho, Ommy Dimples, William Mtitu, Mwana FA na wengine wengi.
Mke wa mwigizaji Sajuki Bi! Wastara Juma ambaye ni mwigizaji pia, akitoa shukrani kwa wasanii na watanzani kwa mchango mkubwa alioupata katika matibabu ya mumewe, na pia alielezea maudhui ya filam ya SAYLA iliyoiandaliwa na wasanii wa filamu hapa nchini, akiwa nchini India kwa matibabu, amesema kuwa inalenga kumsaidia Sajuki kimatibabu zaidi kwani ingawaje hali yake inaendelea vyema lakini bado anahitaji matibabu madogomadogo, ili kuweza kuimarisha afya yake.
Mkurugenzi  mtendaji wa Fullshangwe Blog, Bw. John Bukuku akimkabidhi mke wa Sajuki, Wastara Juma kiasi cha Sh. laki moja 100,000, kama sehemu ya mchango wake kwa ajili ya matibabu ya Mumewe.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat