Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
UCHOVU uliishika Italia, huku pia ikikumbwa na majeruhi na kulazimika
kumaliza mchezo na watu 10 uwanjani. Haikuwa na majibu mbele ya
Hispania katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya Jumapili
usiku.
Hata mkali Mario Balotelli safari hii hakuweza kuikoa
Azzurri na kipigo cha mabao 4-0, ambacho ni cha kwanza kutokea katika
mchezo wa fainali ya michunao hiyo tangu mara ya mwisho Ujerumani
Mashariki wakati huo ilipoifunga Urusi mabao 3-0 mwaka 1972.
Italia
haikuwa miongoni mwa nchi zilizopewa nafasi ya kutwaa ubingwa.
Ilishiriki michuno hiyo, huku ligi ya nyumbani ikiwa kovu la kashfa ya
rushwa na upangaji matokeo.
Lakini pamoja na hayo, imepambana na kumaliza katika nafasi ya pili, pengine hawana sababu ya kujutia.
''Ulikuwa
mchezo mkubwa kwetu mwaka huu," alisema Kocha wa Italia Cesare
Prandelli. "Jambo la kujutia kufungwa kwetu, ni kwamba hatukuwa na
nafasi zaidi ya kujipanga, tulikwenda uwanjani tukiwa nguvu tofauti na
washindani wetu.''
Lakini Prandelli alikasirishwa kuona kikosi
chake kikiwa na watu nane nyuma kikishindwa kuondoa hatari na kupelekea
bao la kwanza dakika ya 14 likifungwa na David Silva.
Dakika saba
baadaye, beki wa kutegemewa Italia Giorgio Chiellini alijitonesha misuli
ya nyuma ya goti, tatizo alilowahi kupata kwenye mchezo dhidi ya
England robo fainali.
Kiungo Daniele De Rossi, ambaye alilazimika kutoka kwenye mchezo dhidi ya England, alicheza bila kuwa fiti kwa asilimia 100.
'Tulipobaki
10 uwanjani tusingeweza kufanya lolote," alisema Prandelli.
''Tulijaribu kurejea kwenye mchezo kipindi cha pili, lakini
tulipompoteza Thiago Motta mechi ilikuwa imekwisha kwetu.''
Nafasi ya Motta ilichukuliwa na Riccardo Montolivo dakika nne zilizotangulia.
''(Montolivo) alikuwa amechoka sana," alisema Prandelli. Kwa ufupi, sehemu yote ya kiungo chetu ilikuwa imechoka.''
''Lakini pamoja na kupoteza, ni lazima tufahamu kwamba tulichofanya kinastahili pongezi, tulionyesha uwezo kwenye mashindano."