Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa, Aggrey
Mwanri amesema maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara
yaliigharimu Serikali kiasi cha Sh27.5 bilioni.
Mwanri alisema kiasi
hicho kilipunguzwa baada ya kubana matumizi ambapo awali bajeti ya
maadhimisho hayo ilikuwa Sh30 bilioni kwa matumizi ya wizara , mikoa,
mamlaka za Serikali za mitaa na taasisi mbalimbali.
Mwanri
alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Wawi, (CUF) Hamad Rashid Mohamed,
aliyehoji kuhusu gharama za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru na
uwezekano wa Serikali kufanya sherehe moja ili kubana matumizi kwa ajili
ya matumizi mengine ya maendeleo kama madawati na vifaa vya elimu.
Mwanri
alisema kumbukumbu hii ni ya muhimu kwa taifa kwa faida ya Watanzania
hasa katika kukijengea uzalendo kizazi cha sasa ambapo hakikuwapo wakati
uhuru uliopatikana.
“Maadhimisho haya ya kihistoria yameisaidia
nchi yetu kujitangaza nje ya nchi na kujiletea sifa kubwa na pia
kuvutia wawekezaji na watalii,” alisema Mwanri.
Aidha Mwanri
alisema ilikuwa ni jambo la msingi kwa taifa kufanya maadhimisho hayo
kwa sababu ya umuhimu wa historia katika taifa lolote.
“Sherehe zilifanyika katika maeneo yote hayo ili kuwafanya Watanzania waijue nchi yao ilipotoka,”
Waziri huyo aliongeza kuwa, nchi isiyo na historia ni kama imekufa kwani watoto wa sasa wanatakiwa wajue historia yao.
July 3, 2012
WAKARI TUKILALAMIKIA UKATA: Serikali ilitumia Sh 27 bilioni kwa sherehe za Uhuru
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget