Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
TUME ya Mabadiliko ya Katiba imesema kuwa itafanya marekebisho ya
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa awamu, ili kutoa ufafanuzi wa jinsi
ya upatikanaji wa Viongozi na Wawakilishi wa wananchi katika Bunge la
Katiba.
Vifungu vitakavyofanyiwa marekebisho na tume hiyo
inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba ni pamoja na kifungu cha 22 na
kifungu kidogo c, cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.Akizungumza katika
hafla iliyojadili Sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyoandaliwa na Umoja
wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahiliso), Naibu Katibu wa Tume hiyo Casmir
Kyuki alibainisha hayo akisema marekebisho hayo yatafanyika kwa awamu na
kwamba hii itakuwa ni awamu ya pili kufanyika.
Alisema licha ya
kuwepo kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayoeleza mambo mbalimbali
yanayohusu mabadiliko ya sheria hiyo, baadhi ya vifungu vitafanyiwa
marekebisho ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wananchi.
"Katika
sheria hii kifungu cha 22 pamoja na kifungu kidogo cha C, vitafanyiwa
marekebisho kwa awamu, ili kusaidia kutoa ufafanuzi kwa wananchi,
kutambua jinsi viongozi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali
watakavyotoa wawakilishi katika Bunge la Katiba," alisema Kyuki na
kuongeza:
"Watu wanaweza kuuliza maswali kwa jinsi gani
watashiriki katika Bunge la Katiba kwani Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
kifungu cha 22 na kifungu kidogo C vimeeleza, lakini marekebisho
yatafanyika kuwezesha kutoa ufafanuzi zaidi katika kipengele hicho."
Akizungumzia
ushirikishwaji wa Makundi Maalumu katika mchakato wa upatikanaji wa
Katiba mpya, mtoa mada kutoka tume hiyo Said Nzori alisema kuwa makundi
hayo yanawakilishwa na viongozi wake kwa kuwa wao pia wanakutana katika
vyama vyao na kwamba wao pia wanapaswa kushiriki katika mchakato huo wa
utoaji maoni.
Alisema kuna taasisi na vyombo mbalimbali vya watu
walio katika makundi maalumu nao hukutana na kujadili masuala ya
upatikanaji wa Katipa mpya na kutokana na sheria hizo watashiriki
kupitia wawakilishi wao.
"Tume inachoweza kusema ni kwamba uamuzi
unaotolewa na watu walio katika makundi maalumu wanapokutana yafikishwe
kwenye Tume ya Marekebisho ya Katiba kupitia wawakilishi wa vyama vyao
au taasisi ili yafanyiwe kazi,"alisema Nzori.
Katika mjadala huo
washiriki kutoka vyo vikuu mbalimbali walisema ni vyema wafugaji na
wakulima wakapewa pia elimu ili waweze kutoa maoni yao ipasavyo.
Akifunga
kongamano hilo, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba,
alisema wasomi nchini wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhamaisha wananchi
kushiriki kutoa maoni ya Katiba mpya.
Alisema tume yake
itahakikisha wananchi wote wanapata nafasi ya kushiriki kikamilifu,
kutoa maoni yao na kwamba hawawezi kukubali kushindwa kufanikisha kazi
waliyopewa.
"Wasomi mnatakiwa kuwa mastari wa mbele kuhakikisha
mnahamasisha wananchi wote kushiri kutoa maoni yenu na tume
itajitahidi kufanikisha kazi hiyo kwa kupitia maeneo yote nchini ili
wanachi washiriki kikamilifu," alisema Jaji Warioba.
July 4, 2012
Tume:Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kurekebishwa kwa awamu
Millionfortune.com
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget