********
JUMLA
ya warembo 15 wamejitokeza kuwania taji la Mrembo wa Sinza “Redds
Miss Sinza 2012” yaliyopangwa kufanyika julai 13 kwenye ukumbi wa
Mawela social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican
City.
Washiriki wa Redds miss sinza 2012
Mratibu
wa mashindano hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment
aliwataja warembo hao kuwa ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu
Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Esther Mussa, Christina
Samwel, Nahma Said, Shadya Ali, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi,
Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Majuto
alisema kuwa warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu
Juma ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model.
Alisema kuwa mazoezi ya warembo hao yanafanyika kwenye ukumbi wa
mashindano hayo, Mawela social kuanzia saa 8.30 mchana.
“Warembo
wamepania kufanya kitu cha kihistoria siku ya mashindano nah ii
inatokana na ukweli kuwa wamejiandaa vilivyo na kwa sasa wanamalizia tu
baadhi ya vitu vidogo vidogo vya mashindano hayo, alisema Majuto.
Alisema
kuwa lengo kubwa la mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds
Miss Tanzania mbali ya taji la Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo
lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion,
Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.
“Tuna
warembo moto wa kuotea mbali ambao kwa sasa wameonyesha kupania
kufanya kile ambacho kimesubiliwa na wadau wa warembo wa mitaa ya Sinza
na vitongoji vyake, hii inatokana na ukweli kuwa mashindano haya ni ya
mwisho kwa upande wa vitongoji jijini,” alisema.